Mwanafunzi James Paulo (17) anayesoma shule ya msingi Mandera halmashauri ya Chalinze Bagamoyo Pwani, ameliwa na mamba katikati mto Wami, alipokuwa anavua samaki.
Akizungumza na Waandishi wa habari mjini hapa, Ofisa Wanyama Pori halmashauri hiyo Revocatus Samuel alisema kuwa, tukio hilo limetokea Jumatatu ya Aprili 8 saa 6 mchana, akiwa na wenzake walipokwenda kuvua kwenye mto huo.
"Akiwa na wenzake katika zoezi la uvuvi, ghafla alitokea mamba akamvutia kwenye maji, hali iliyosabaabisha taaruki kubwa kwa vijana wenzake, ambao walikimbilia kwa viongozi wa Serikali kutoa taarifa hiyo," alisema Samuel.
Ofisa hiyo aliongeza kwamba baada ya tukio hilo msako mkali ulianza wa kumtafuta mwanafunzi huyo ili kuokoa maisha yake, lakini zoezi hilo halikufanikiwa, mpaka siku ya pili yake mabaki ya mwili huo yalipopatikana kwenye kijiji cha jirani cha Mkoko.
Ofisa hiyo aliongeza kwamba mwanafunzi hiyo ambaye kwa sasa ni marehemu, alikuwa mkazi wa Kijiji cha Kibaoni Kitongoji cha Maraha Kata ya Mandera, ambapo masalia ya mwili wake yamezikwa juzi usiku kijijini hapo.
"Tayari tumeshapeleka askari wa Wanyamapori kwa ajili ya kujaza fomu kuipatia kifuta machozi familia, huku elimu kwa wananchi ikiendelea za namna ya kujilinda na wanyama hao wakali," alisema Samuel.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mandera Madaraka Mbonde ameelezea lusikotishwa kwake kutokana na tukio hilo, huku akieleza kwamba ndani ya miaka mitatu, tukio hilo ni la tatu la kuliwa wakazi kwa mamba.
"Elimu inayoendelea kutolewa imekuwa msaada mkubwa, kwani kwa sasa matukio hayo yameanza kupungua mpaka tukio la kijana wetu la juzi ni la kwa kipindi cha miaka mitatu," alisema Mbode.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo