Mwanamke Apigwa na Kunyolewa Nywele na Mumewe Baada ya Kutaa Kucheza Dansi

Mwanamke Apigwa na Kunyolewa Nywele na Mumewe Baada ya  Kutaa Kucheza Dansi
Mwanamke mmoja raia wa Pakistani amemshutumu mume wake hadharani kwa kumpiga na kumnyoa nywele baada ya kukataa kucheza mbele za mwanaume huyo na rafiki zake, Kesi ambayo imeleta maswali mengi kuhusu usalama wa wanawake nchini humo.

Asma Aziz, kutoka jimbo la Lahore, alisababisha kuzungunzwa kwenye vichwa vya habari vya vyombo mbalimbali baada ya kusambaza video kwenye mitandao ya kijamii akionyesha kichwa chake kilichonyolewa na uso wenye alama zilizotokana na vipigo.

Mume wake, Mian Faisal, na msaidizi wote wanashikiliwa na polisi.Bwana Faisal amekana kumtesa mkewe.

Hatahivyo,tukio hilo limeamsha hisia kali na kutolewa wito kuwa hatua zaidi zichukuliwe ili kukomesha unyanyasaji.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Shirika la Amnesty International limesema mabadiliko ni lazima.

, bi Aziz alidai kuwa siku mbili zilizopita aliteswa baada ya kukataa kucheza muziki mbele ya marafiki wa muewe ambao walifika nyumbani kwao.

''Alinivua nguo mbele ya wafanyakazi wake.Wafanyakazi walinishika wakati akininyoa nywele na kuzichoma.Nguo zangu zilijaa damu.Nilikua nimefungwa, akatishia kunining'iniza nikiwa mtupu,'' alieleza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad