Sokwe mtu wasimama kupiga picha na Askari wanyama pori
0
April 23, 2019
Katika hali ya taharuki sokwe mtu wawili wameishangaza dunia baada ya kusimama ili wapigepicha kwa simu iliyo na kamera ya mbele na binadamu ambaye ni askari wa wanyama pori nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC).
Sokwe hao wamepiga picha ya selfie na askari huyo, ambaye aliwahi kuwaokoa kwenye makucha ya majangili walipokuwa wadogo baada ya wazaziwao kuuawa.
Kwa mujibu wa Naibu mkurugenzi wa makao ya sokwe yatima kwenye hifadhi ya Taifa ya Virunga nchini DRC, Innocent Mburanumwe ameliambia shirirka la habari la BBC kuwa sokwe hao walijifunza kuiga tabia za binadamu wanao watunza tokea walipokuwa wadogo.
Sokwe hao wamejijengea imani kuwa askari ni wazazi wao kwani mamazao waliuawa mwezi julai 2017 na wakaanza kulelewa na binadamu wakiwa na umri kati ya miezi miwili na minne.
Mburanuwe ameongeza kuwa walianza kujifunza na kuiga tabia za binadamu taratibu ambapo kwa sasa wanaweza kusimama kama walivyoonekana kwenyepicha japo hali hiyo haitokei kila wakati.
Hifadhi ya Viruga ipo mashariki mwa DRC eneo ambalo limetawaliwa na vita baina ya Serikali na makundi kadhaa ya waasi, tokea mwaka 1996 jumla ya askari wanyamapori 130 wameuawa na majangili.
Tags