"Napata Mshahara wa Kukaa na Mchepuko" - RC Mbeya

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema yeye ataendelea msimamo wake katika kuhakikisha anasimamia sheria ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika katika jiji la Mbeya.

Akizungumza jijini Mbeya, Mkuu huyo wa Mkoa amesema amekuwa akiingia majaribuni mara kwa mara hususani kupitia watu wenye vipato vikubwa kwa nia ya kumuhonga lakini amekuwa akiwaagiza wapeleke fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo.

"Tukisiamamia sheria tutalifikisha taifa hili mbele, inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wanaleta unafki katika kusimamia sheria hii sio nzuri hata kidogo", amesema Chalamila.

"Tangu Rais Magufuli aliponiteua sijawahi kukaribisha kiumbe chochote kije kinipe utajiri mfukoni mwangu, watu walionesha nia, nikawaambia wapeleke kwenye mashule lakini mshahara unaonipa napata mshahara wa kukaa na hata mchepuko kidogo", ameongeza Albert Chalamila.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mara kwa mara amekuwa akiingia kwenye mvutano wa maneno na Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) ambapo mara nyingi imekuwa ikisababishwa na mivutano ya kisiasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad