Ndugai: Askari Akikisha Wabunge Wote Waliosusia Bunge na Kutoka nje Hawarudi Tena Bungeni

Spika wa Bunge Ndugai amewaagiza maaskari wa Bunge kuhakikisha wabunge wote waliosusia kikao cha Bunge na kutoka nje hawarudi Bungeni tena kwa siku ya leo.

Wabunge hao wametoka mara baada ya Kamati ya Bunge ya Kinga, Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kumtia hatiani Mbunge huyo  kwa kudharau Bunge kwa kuita Bunge ni dhaifu na hivyo kamati imeazimia Lema kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia leo.

"Hawa wabunge wanaosusa vikao huku ndani wakitoka nje waandishi wanawakimbilia kuwahoji. Sasa napiga marufuku. Mwandishi yeyote atakayeonekana nje ya ukumbi wa Bunge anamhoji mbunge aliyesusa kikao, atanyang'anywa kitambulisho na hataruhusiwa kuripoti habari za bunge wala hatakanyaga tena hapa" amesema Spika.

Mkutano wa 15 wa Bunge ulianza April 02, 2018 Jijini Dodoma ambapo wastani wa maswali 515 ya kawaida yataulizwa na kujibiwa na serikali. Aidha, wastani wa maswali 88 ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku ya alhamisi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad