Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwili wa aliyekuwa Ofisa wa Wizara ya Madini, Mery Mkwaya Maramo aliyefariki mwanzoni mwa wiki hii na kuzikwa jana katika makaburi ya Pugu-Mwakanga jijini Dar es salaam, umefukuliwa na kutolewa nje ya jeneza kisha kuvuliwa nguo usiku wa kuamkia leo-
Ijumaa, Aprili 12, 2019 na watu wasiojulikana.
Akizungumzia tukio hilo, Kaka wa marehemu Mary aitwaye Deogratius Maramo, amedai mwili wa marehemu ulitolewa nje na umekutwa umechanuliwa miguu, lakini bado wanasubiri ripoti ya polisi ili kujua kilichotokea kwani hakuna kitu chochote kilichoibiwa katika kaburi hilo.
Mramo anasema kuwa baadaya kufika makaburini hapo walifika kwa mwenyekiti wa mtaa ule ili kutoa taarifa ambapo hata wenyeji wa eneo hilo walishangazwa na kitendo hicho na kuhusisha tukio hilo na imani za kishirikina.
Kwa upande wake mwangalizi wa sehemu ya makaburi hayo ambayo yanamilikiwa na Kanisa Katholiki, Mzee Hela Mwenzigeje amesema kuwa kitendo hicho ni mara ya kwanza kutokea katika eneo hilo na kimewatia doa.
Aidha wakazi wa eneo hilo wameomba watu wa Kanisa waweke uzio katika eneo hilo ili kuondoa wasiwasi uliotanda miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.