Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hawezi kufika mkoani Mtwara bila kuongelea suala la bei ya korosho kwani na yeye ni mtoto wa mkulima.
Leo Rais Magufuli anaweka jiwe la msingi la Upanuzi wa Uwanja wa ndege wa Mtwara na yupo katika ziara ya siku tatu Mkoani Mtwara.
"Mimi mlinichagua kwa kura zenu nilikuwa na wajibu wa kuwatetea kama Kiongozi niliona serikali kuna hela nikasema kwanini nisinunue kwa shilingi 3300 kwa Korosho zote zilizopo kutoka kwa Kilimo na huo ndiyo Uongozi," amesema.
"Nimeagiza hapa ziletwe zaidi ya bilioni 50 wote tuwalipe ila wale ambao wana Kangomba wakikiri wamenunua kwa watu zikachukuliwa na watu hawana mashamba naomba muwalipe kama wakikiri makosa yao," amesema.
Ameendelea kwa kusema, 'Wapo watu ambao hawajalipwa si kwasababu hawastahili hii imetokana kuna baadhi ya akaunti ambazo majina ya akaunti hayakulingana wapo ambao waliwasilisha akaunti za shangazi zao ndugu zangu hela za serikali kutoka zina utaratibu wake.
Nilichaguliwa kwa Kura Zenu, Nilikuwa na Wajibu wa Kuwatetea - Rais Magufuli
0
April 02, 2019
Tags