Nyota wa timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, Kelvin Pius John kwa jina la utani ‘Mbappe’ amezungumzia mipango yake na staaa wa timu ya taifa ya Cameroon na klabu ya Barcelona, Samuel Eto’o huku akielezea sababu kubwa zilizopelekea kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Afcon 2019 iliyomalizika hapo jana siku ya Jumapili hapa nchini Tanzania.
Akizungumza na Radio Metro FM ya jijini Mwanza, Kelvin John amesema kuwa mashindano ya Afcon ni magumu ukilinganisha na hayo mengi ambayo waliyowahi kucheza hapo kabla.
”Mashindano ya Afcon ni magumu sana kushinda yote ambayo tulishawahi kucheza huko nyuma, tumecheza CECAFA, COSAFA haya yote tumecheza katika ukanda wa Afrika Mashariki ama Kusini, lakini Afcon tumekutana na ukanda tofauti,” amesema Kelvin mchezaji wa Serengeti Boys.
Kelvin ameongeza ”Mechi nyingi za kirafiki hatukucheza na ukanda wa Magharibi ama Kaskazini, tulikuwa tukicheza na ukanda wa Afrika Mashariki ama Kusini, kwahiyo walitupa wakati mgumu.”
”Tuliyokuwa nao kwenye group letu, ambaye tulikuwa naye kwenye ukanda wetu ni Uganda peke yake, kingine wenzetu walichotuzidi ni kwamba wapo vizuri kwenye ‘physics’, tofauti na sisi tuna miili midogo na ‘physics’ yetu ndogo, tulizidiwa hapo.”
”Nilichojifunza ni kwamba wenzetu wanambinu, mechi ya kwanza tulivyocheza na Nigeria tulikuwa tunaongoza lakini baadhi ya wachezaji wa Nigeria wakawa wanaitana wenyewe, wakaanza kucheza kila mtu ‘individual’, kwa uwezo binafsi ili kuweza kubadilisha matokeo, sisi tukataka kucheza kwenye mfumo ule ule ambayo tulifunzwa na mwalimu.”
Image result for kelvin john serengeti boy
Akizungumzia mipango yake na aliyekuwa nyota wa klabu ya Barcelona, Samuel Eto’o, Kelvin amesema alimuahidi kufuatilia mechi zake.
”Aliniambia sijawahi kukuona lakini ntafuatilia mechi zako zote utakazoanza kucheza sasa hivi, ongeza juhudi nimeona mechi yako moja ambayo umecheza na Rwanda na nilivutiwa na wewe.”
”Nakuahidi kwenye mashindano ya Afcon ambayo yatafanyikia hapa nchini kwenu kama utafanya vizuri, ntakupa ofa ya kwenda timu kubwa yoyote nchini Ufaransa, wanaonisimamia wapo kwenye mazungumzoa na timu nyingi na mimi nipo tayari kucheza.”
”Juzi nimetoka kuwasiliana naye ameniambia amenifatilia kwenye mashindano haya na amevutiwa na mimi na yupo kwenye mazungumzo na ya mwisho kuona watanipeleka kwenye klabu gani.”
”Kabla ya Afcon niliambiwa kuna timu tano ambazo zinanifuatilia baada ya mashindano tutazungumza nao niende, baada ya kuambiwa hivyo nikaomba nisiambiwe yote ili yasiniathiri kisaikolojia.”
Kelvin amewahi kwenda nchini Denmark katika program ya maendeleo ya kimichezo na timu ya HB Koge inayoshiriki ligi kuu nchini humo. Lakini pia amewahi kuwa mchezaji bora wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Nyota wa Serengeti Boys Kelvin John ‘Mbappe’ afunguka dili lake na Samuel Eto’o
0
April 29, 2019
Tags