Papa Francis Apiga Goti na Kubusu Miguu ya Salva Kiir na Machar

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amefanya tendo la unyenyekevu na ambalo halikutarajiwa baada ya kupiga magoti na kubusu miguu ya viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini, kuwahamasisha kuuendeleza mchakato wa amani.


Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, Mwishoni mwa ziara ya kiroho ya siku mbili ya viongozi hao wa Afrika mjini Vatican, Papa Francis alimuomba rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na hasimu wake Rieck Machar kuendeleza mazungumzo ya amani, licha ya kuongezeka kwa ugumu, na kisha alipiga magoti na kubusu miguu yao, pamoja na ya makamu wa rais Rebecca Nyendeng Garang.


Papa Fransic hufanya tendo la kitamaduni la kiimani la kuwaosha miguu wafungwa siku ya Alhamisi kuu, lakini hajawahi kufanya tendo kama hili kwa viongozi wa kisiasa.


Alisema mwishoni mwa ziara hiyo kwamba anataraji kusitishwa kwa uadui, mapigano, mgawanyiko wa kikabila na kurejeshwa kwa hali ya amani nchini humo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad