Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola ameshangazwa na onyo lililotolewa na Ole Gunnar Solskjaer kwa wachezaji wa Man United kwamba wajiandae kuchezewa rafu katika uwanja wa Old Trafford siku ya Jumatano.
Siku ya Jumanne Solskjaer alisema: Kutakuwa na uchezaji rafu , watawagonga visigino vyenu na kuwapiga mateke.
''Je alisema hivyo? huku tukiwa na asilimia 65 na 75 ya mchezo anawezaje kusema hivyo?'', alisema Guardiola.
''Sipendi, kikosi changu hakikuundwa kucheza rafu, sipendi kabisa''.
Guardiola hapo awali amekana madai kwamba yeye hushauri kikosi chake kucheza vibaya ili kuzuia mashambulizi ya upinzani.
Kibinafsi City haijafurahia matamshi hayo ya Solskjaer kuhusu swala hilo hususan kwa sababu takwimu hazimuungi mkono raia huyo wa Norway.
Kulingana na Opta, City imesababisha fauli 170 bila kushirikisha mipira ya kuotea katika eneo la upinzani kufikia sasa msimu huu .Cha kushangaza ni kwamba United imesababisha fauli 195.
Tukiongezea, kwa jumla wachezaji wa City wamepokea kandi 38 za njano na nyekundu moja katika ligi ya Premia msimu huu huku wachezaji wa United wakipokea kadi 64 za majano na nne nyekundu.
''Katika misimu 10 kama mkufunzi sijawahi kujiandaa kwa mechi nikifikiria vitu kama hivyo , hapana sijawahi'' , alisisitiza Guardiola.
Katika soka mara nyengine unalazimika kufanya makosa kama hayo. Lakini sijawahi kuwashauri wachezaji wangu kuwaadhibu wapinzani.
Pengine baada ya mechi mutamuuliza katika mkutano na vyombo vya habari.
Mnamo mwezi Novemba , Guardiola alipewa onyo rasmi na shirikisho la soka FA kwa kuzungumza kuhusu refa Anthony taylor kabla ya mechi ya debi ya awali katika uwanja wa Etihad ambayo Cituy ilishinda kwa mabao 3-1.
Mnamo mwezi Oktoba mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez alipigwa faini ya £60,000 kwa matamshi aliyotoa kuhusu Andre Marriner kabla ya mechi ya sare ya bila mabao dhidi ya Crystal palace.
Marinner ndiye atakayesimamia mechi ya Old Trafford na huku sheria za FA zikiwazuia wakufunzi kuzungumzia kuhusu marefa kabla ya mechi , Solskjaer karibu awekewe vikwazo wakati aliposema: City huwapeleka mbele wachezaji wengi na unaweza kuona kwamba wako mbele ili kujaribu kushinda mipira na kufanya fauli.
Pep Guardiola achukizwa na matamshi ya Ole Gunnar Solskjaer
0
April 24, 2019
Tags