Rai Yatolewa Kwa Jamii Kutowanyanyapaa Au Kuwabagua Wagonjwa Wa Afya Ya Akili Kwa Imani Za Kishirikina

Rai imetolewa kwa jamii kutowanyanyapaa au  kuwabagua wagonjwa wa akili kwa imani za kishirikina na badala yake wapewe huduma stahiki za kibinadamu pindi wanapokutwa wakizagaa  na kuzurura mitaani.

Rai hiyo imetolewa jana  April 18,2019 ,Bungeni  jijini Dodoma Naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Dokta. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la mbunge wa Njombe mjini , Mhe.Edward  Frans Mwalongo liliohoji serikali ina mpango gani wa kuwahudumia wagonjwa wa akili wanaozurura mitaani katika mavazi ,matibabu na makazi huku mbunge wa Rombo ,Joseph Selasini akihoji juu ya kufufua vituo vya ushauri nasaha kwa wagonjwa wa akili.

Katika majibu yake , Dokta.Ndugulile amesema  magonjwa ya akili yanatibika na huduma hizo zinatolewa bure hivyo ameiasa jamii kuacha tabia ya kuwanyanyapaa na kuwabagua kwa imani za kishirikina na badala yake wawaibue pindi wanapowaona na kuwapeleka katika vituo vya Afya.

Hata hivyo,Naibu waziri Ndugulile ameezea jinsi wizara ilivyojipanga kutoa huduma za Afya huku akizungumzia juu ya sheria ya Afya ya akili ya mwaka  2008  sehemu ya 3 kifungu cha sheria No.9 Kifungu kidogo cha kwanza hadi cha tatu kinaeleza wazi juu ya jukumu la maafisa polisi,maafisa usalama,maafisa ustawi wa jamii ,viongozi wa dini,maafisa watendaji wa kata na vijiji  jukumu la kumchukua mtu yeyote anayerandaranda  na kumfikisha sehemu ya uchunguzi wa magonjwa ya akili na ikithibitika taratibu za matibabu huanza mara moja .

Dokta Ndugulile anavitaja visababishi vya magonjwa ya  afya ya akili ikiwa ni pamoja na kurithi,matumizi ya dawa za kulevya,  na hali ya maisha ambayo hupelekea msongo wa mawazo ambapo kwa sasa kuna wimbi la ugonjwa wa Sonona.

Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro ni miongoni mwa Wilaya zenye magonjwa ya akili kwa wingi hususan ugonjwa wa kifafa huku wizara ya Afya  ikiendelea kufanya utafiti juu ya tatizo hilo na Watafiti wasema mmoja kati ya wagonjwa 10 wa maradhi ya akili ni kutokana na kuvuta bangi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad