Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameifokea nchi ya Canada kwa kushindwa kuchukua hatua juu ya takataka ilizosafirisha hadi katika nchi yake iliyopo kusini mashariki mwa Asia miaka kadhaa uliopita.
Nchi hiyo imewasilisha mara kadhaa mamamiko yake kupinga kidiploamasia hatua ya Canada ya kutuma tani za uchafu nchini Ufilipino kati ya mwaka 2013 na 2014.
Wiki hii rais Duterte alitishia kurejesha takataka hizo nchini Canada.
Canada inasema "ina nia sana "ya kutatua swala hilo na itashirikiana na Wafilipino kufanya hivyo.
Rais Duterte aliikosoa Canada juu ya mzozo huo wa muda mrefu wa kidiplomasia , akisema imeibadilisha nchi yake saying it is kuwa "dangulo la kutupa uchafu".
"kuhusiana na taka za Canada , ninataka maboti yaandaliwe ," alisema Jumatatu, na kuongeza kuwa : "ni bora wavute hicho kitu nje ya nje yetu au nipeleke meli za uchafu wao huko''.
"ngoja tupambane na Canada. Nitatangaza vita dhidi yao."
Rais Duterte anafahamika kwa mtindo wake wa kutoa kaulli za wazi na mara nyingi hutumia lugha na kauli kali zenye utata.
Kauli zake za Jumatatu zilihusu kontena zilizotumwa kwa meli katika mji mkuu Manila,na kampuni ya kibinafsi ya Canada kwa ushirikiano na wadau wau wa Ufilipino.
Duterte: Sikukusudia kumshambulia Obama
Serikali mjini Manila inasema makontena hayo yaliyowasili katika bandari ya kimataifa ya Manila , yaliwekwa utambulisho gushi, ambapo yaliandikwa kuwa yalikuwa na plastiki ambazo zingetumiwa kutengeneza bidhaa nyingine , lakini ukweli ni kwamba yalikuwa yamesheheni vifaa vikuukuu mbali mbaloi vya nyumbani.
Uchunguzi ulibaini kuwa baadhi ya makontena yalikuwa na chupa za plastiki na mifuko, takataka za nyumbani na nepi za watu wazima zilizotumiwa(diapers).
Uchunguzi mwingine iwa kontena zilizosalia 2015 ulibaini kuwa zilikuwa na uchafu mwingine usio hatari , zikiwemo taka za nyumani na mitaani.
Rais Duterte Ufilipino Aikemea Canada "Ufilipino Sio Dangulo la Taka la Canada''
0
April 24, 2019
Tags