Rais Magufuli Ataja Idadi ya Viwanda Vilivyojengwa Toka 2015


Rais John Magufuli amesema kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kilikuwa hakifanyi vizuri ndio maana akakipeleka chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, lakini kama kitaendelea hivyo atakiweka chini ya Ofisi yake.

Amebanisha hayo kwenye ziara mkoani Njombe ambapo amesema viwanda vinahitajika, hivyo mamlaka zote zinazohusika ziendeleeni kuhamasisha uwekezaji katika Sekta ya viwanda, huku ikitengenezwa mikakati ya kulinda viwanda vilivyojengwa tayari.

"Nimefurahi kusikia kiwanda kimetoa Milioni 250 kwa ajili ya kuchangia shughuli za kijamii pamoja na azma yao ya kutaka kuwafundisha wakulima wa chai mbinu za kisasa za kilimo hicho," amesema.

"Jumla ya viwanda 3500 vimejengwa nchi nzima tangu niingie madarakani mwaka 2015," amesema Rais Magufuli.

Ameendelea kwa kusema, 'Mtu akija anataka kuwekeza, kesho yake apewe eneo aanze kuwekeza, ni lazima twende na kasi hiyo. Mtu anataka kujenga kiwanda chake anatafuta ardhi mara sijui kuna NEMC sijui kuna OSHA, unaosha nini?, we umelikuta liardhi la Mungu hapo unaangalia sijui sijui! kuna vibali vya hovyo, tunajichelewesha wenyewe'.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad