Rais TFF aihofia Senegal, asema hana shaka na Algeria, Kenya
0
April 14, 2019
Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Walace Karia amesema kundi C ambalo Tanzania imepangwa sio kundi gumu lakini pia sio kundi rahisi na mechi itayoweza kuwa ngumu ni ile dhidi ya Senegal kwani wawili hao hawajawahi kukabiliana ndani ya dimba moja.
Ameongezea kuwa endapo Tanzania itajipanga vyema bado ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri na kupata matokeo mazuri.
”Mechi ambayo naona itakuwa ngumu lakini pia wachezaji wetu wakijitahidi tunaweza kupata matokeo ni mechi ya Senegal, lakini hizi mechi nyingine kwakuwa tumecheza nao mara kwa mara mimi nadhani ile hofu itakuwa imepungua na tunaweza kupata matokeo” amesema Wallace.
Kundi C Tanzania imepangwa na timu ya Senegal, Kenya na Algeria.
Kwa upande wa Algeria na Kenya Wallace amesema kuwa hana shaka nazo sana kwani tayari wamewahi kukabiliana na baadhi ya mechi walifanikiwa kutoka dro.
”Kundi sio rahisi lakini pia sio gumu, Algeria tumecheza nao mara kwa mara na wametufunga sana ingawa mechi ya mwisho tulitoka nao dro, mi najua wataingia watatudharau na watu wetu wakiwa vizuri tutaweza kupata matokeo, Kenya tunacheza nao mara kwa mara nao pia ni wapinzani wetu, na hata mechi ya mwisho tuliyocheza tulitoka dro” amesema Wallace
Naye Khamis Abdalah Said Kaimu Rais wa ZFA amesema Tanzania yupo kwenye kundi ambalo si gumu sana tukijikaza tunaweza tukaingia kwenye makundi, kwa hiyo amewaomba wachezaji, wananchi kwa jumla na makocha kusimama kama watanzania na kuhakikisha tunashinda kwani uwezo huo upo.
Aidha mchuano wa AFCON 2019 kuna makundi sita ambapo kundi A likiwa na timu ya Egypt, DR Congo, Uganda, Zimbabwe; Kundi B likiwa na timu ya Nigeria, Guinea, Madagascar, na Burundi; Kundi D likiwa na timu ya Morocco, Cote D’Ivoire, South Africa na Namibia; Kundi E likiwa na Tunisia, Mali, Mauritania, Angola na Kundi F likiwa na Cameroon, Ghana, Benin, Guinea Bissau
Tags