Rais wa DR Congo Azuru Marekani

Rais wa DR Congo azuru Marekani
Rais wa DR Congo, Felix Tshisekedi Tshilombo yuko ziarani tangu Jumatano wiki hii jijini Washington, nchini Marekani, kwa ziara ya siku mbili hadi Aprili 5 mwaka huu.

Felix Tshisekedi amechagua Marekani kwa ziara yake rasmi ya kwanza nje ya bara la Afrika tangu alipochukuwa hatamu ya uongozi wa nchi.

Hata hivyo, hakutakuwa na mkutano kati ya rais huyo na Donald Trump. Lakini, kwa mujibu wa Jason Stearns, "hakuna haja ya kutafsiri hali hiyo kama pigo kwa Felix Tshisekedi".

Tshisekedi anakutana na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, pia anatarajia kukutana na Seneta Cory Booker; na kutakuwa na mikutano mingi yenye lengo kubwa kuhusu uwekezaji katika sekta ya kibinafsi.

Hata hivyo kwa mujibu wa mtafiti, Felix Tshisekedi anajua kwamba Marekani inaweza kuwa mshirika wake mkubwa dhidi ya mtangulizi wake Joseph Kabila, lakini uungwaji huu mkono wa Marekani sio masharti. Uungwaji mkono wa Marekani kwa utawala wa Tshisekedi unaendana na matarajio yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad