Rais wa Israel Aanza Majadiliano kabla ya Kumteua Waziri mkuu mpya

Rais wa Israel Reuven Rivlin ameanza mashauriano na wawakilishi wa makundi mapya ya wabunge kabla ya kuamua kumteua waziri mkuu ajaye.

 Mazungumzo hayo ni zoezi la kawaida, kutokana na matokeo ya uchaguzi mkuu wiki iliyopita.

Chama tawala cha Likud pamoja na vyama vya jadi vya kizalendo pamoja na vyama vya siasa kali za dini y Kiyahudi vina wingi wa viti 65 hadi 55 bungeni na vinatarajiwa kuelemea kwa waziri mkuu Benjamin Netanyahu.

Rivlin ameanza mikutano yake leo na maafisa wa chama cha Likud. Baadae atakutana na wajumbe wa vyama vingine 10, kwa utaratibu wa makundi makubwa na kisha madogo, kusikiliza mapendekezo yao, kabla ya kumteua rasmi mgombea anayeamini ana nafasi ya kujenga wingi bungeni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad