RC Akabidhi Matrekta 14 Tabora, Atoa Onyo Kali

RC Akabidhi Matrekta 14 Tabora, Atoa Onyo Kali
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) amekabidhi matrekta 14 kwa vyama vya ushirika vya mkoa huo (Igembesabo) katika hafla iliyofanyika wilayani Igunga mkoani Tabora na kutoa onyo kwa wale watakaoenda kuyaegesha.

Mbali na vyama vya ushirika, Mkuu wa Mkoa amekabidhi Matrekta kwa watu binafsi wakiwemo Mapadri, Maaskofu na Masheikh wa mkoa huo. Amesisitiza matrekta hayo yatumike katika shughuli za kuleta maendeleo kwa mkoa na taifa kwa ujumla. "Sio unachukua trekta unaenda kulipaki.

Trekta hili linaweza kufanya shughuli nyingi za kimaendeleo, hivyo mfanye maendeleo," alisema Mwanri Mbali na kulishukuru Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa mpango wake wa kutoa matrekta kwa wakulima, ameliomba shirika hilo kuchangamkia fursa nyingine za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa Tabora.

"Mkoa wa Tabora una fursa za uwekezaji kwenye wilaya zake zote katika sekta ya nyama, asali, ngozi na tumbaku huku tumbaku ikiongoza kwa 60% kuzalishwa nchini, hivyo nawaomba NDC mje muwekeze kwenye viwanda hivyo," alisema Mwanri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad