Rc Ayoub Awataka Vijana Kuwa Wabunifu

Rc Ayoub Awataka Vijana Kuwa Wabunifu
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka vijana nchini kuwa wabunifu na kutumia fursa mbali mbali zilizopo nchini na kujiendeleza kiuchumi.

Amesema vijana wanatakiwa kuwa mitazamo chanya na kuwa wabunifu katika kazi wanazozifanya kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi na kuimarisha Ustawi wa Jamii.

Wito huo aliutoa wakati wa  hafla maalum ya kusherekea kutimia miaka mitatu ya kikundi cha Wireless Services Group wanajishughulisha na utoaji wa huduma mbalimbali.

Ayoub alisema kuwa vijana wanapaswa kupanua wigo katika kutafuta shughuli za kujiajiri na kuacha mtazamo na fikra   za kutaka kuajiriwa na serikali.

“Vijana wenzangu niwambie kuwa huu si wakati wa kusubiri ajira za Serikali unapaswa kuwa mbunifu na kufikiria nini unaweza kufanya na kuweza kujiajiri wewr mwenyewe” alisema Rc Ayoub.

Alisema hatua hiyo itawasaidia vijana wengi zaidi nchini na kuweza kukuwa katika ustawi ulio bora zaidi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita mapambano dhidi ya dawa za kulevya ambazo zimewaathiri vijana wengi zaidi nchini.

Katika hatua nyingine aliwapongeza kikundi cha Wireles Service Group lkwa kuwakusanya vijana na kujiajiri wenyewe.

“Niwapongeze kwa sababu nyinyi ni baadhi ya vijana muliamua kujiajiri wenyewe na kuungana mkono jitihada za serikali ya mapinduzi ya Zanzibar” alisema Rc Ayoub.

Akisoma risala kwa niaba ya kikundi hicho Rashid Ali alisema lengo la kuanzishwa kwa kikundi hicho ni kutoa ajira kwa vijana mbaliMBALI Nchini.

Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Kariakoo Mjini Magharib Unguja.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad