RPC Arusha Akanusha vifo vya Watu nane


Siku moja baada ya kuenea kwa taarifa katika mitandao ya kijamii juu ya ajali iliyohusisha magari madogo mawiii katika eneo la Oldonyosambu jijini Arusha Kamanda wa Polisi mkoani humo amekanusha taarifa ya vifo vya watu nane na kueleza kwamba vifo vilivyotokea ni vya watu wawili.


Akiwa katika eneo la tukio Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani humo, Jonathan Shana amesema kuwa, jijini humo hakukuwa na mashindano yoyote ya magari kama ilivyo ripotiwa awali na watu waliopoteza maisha mpaka sasa ni watu wawili tu na si watu nane kama ilivyo ripotiwa awali.

"Tukio hili lilionekana kupotoshwa kwa kiasi fulani, taarifa zilizotolewa mitandaoni hazikuwa sahihi. Hakukuwa na mashindano ya magari na waliofariki ni watu wawili tu sio nane", amesema Kamanda Shana. 

Ajali hiyo  iliyo tokea juzi Aprili 21, majira ya saa kumi jioni na kuhusisha magari mawili moja kutoka nchi jirani ya Kenya inatajwa kusababishwa na uzembe wa dereva wa gari lililokuwa katika mwendo mkali huku likijaribu kulipita gari jingine lililokuwa likikata kona bila kuchukua tahadhari ya kutosha.

Samwei Theith ni daktari wa magonjwa ya dharura katika hospitali ya Seliani ya jijini humo baadhi ya majeruhi wametibiwa na kuruhusiwa huku wengine wakiendelea na matibabu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad