Jeshi la polisi Mkoani Manyara katika kipindi cha kushereherekea sikukuu Pasaka limejipanga vizuri kuhakikisha kwamba wananchi Wanasherehekea kwa amani na utulivu na kuwaonya wale wanaofikiria kufanya uhalifu wa aina yoyote ile kwamba watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Jeshi hilo limeeleza kuwa limejipanga kukabiliana na vitendo vyote vya kihalifu na kwamba atakaejaribu kufanya hivyo lazima ashughulikiwe haraka kwa kuwa wamejipanga kikamilifu.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara Augustino Senga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo april 20 2019.
“kutakuwa na doria za magari,miguu katika maeneo mbalimbali ya kumbi za starehe,viwanja vya wazi,katika nyumba za ibada za mkesha kwa hiyo niwahakikishie wananchi kwamba usalama umeimarikana disko toto ni marufuku lakini kama watakwenda katika viwanja vya wazi ruksa nawaonya kwa wale wanaofikiria kufanya uhalifu wa aina yoyote ile nafasi hawana tupo macho na tutawashulikia kikweli kweli”alisema Kamanda.
Aidha kamanda amewataka wazazi katika kipindi hiki cha sikukuu watoto wasitembee pekee yao bali waongozane na watu wazima kuepuka kupotea au kupata madhara yeyote ile sambamba na watu wanapotoka majumbani wasiache nyumba pekee yake wawe na ulinzi jirani kwa kuwa polisi hawatoshi kufikia kila kona.
Kwa upande wa usalama Barabarani amesema jeshi la polisi limejipanga vizuri kuhakikisha usalama unaimarika ikiwemo kuwapima walevi ili kuhakikisha hapatokei ajali zitokanazo na uzembe.
Amewataka madereva na watembea kwa miguu watii sheria bila shuruti na yeyote atakae endesha kwa mwendokasi atachukuliwa hatua kwa kuwa kutakuwa na kamera za kutosha kuangalia mwendo kasi.
Hata hivyo amewaomba wananchi wote kwa ujumla kusherehekea sikukuu hizo kwa amani bila kuleta fujo ya aina yoyote ile kwani jeshi la polisi wapo masaa yote na kama kuna kiashiria chochote cha uvunjifu wa amani watoe taarifa za haraka .
RPC Manyara Atuma Salamu kwa Wahalifu kipindi Hiki cha Pasaka
0
April 20, 2019
Tags