Serengeti Boys imeanza kwa kipigo AFCON U-17 2019
0
April 15, 2019
Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri chini miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys, leo imeanza kucheza mchezo wake wa kwanza wa hatua ya makundi wa fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys leo imeanza dhidi ya Nigeria.
Pamoja na kuwa mwenyeji na kuwa na sapoti ya mashabiki lukuki, Serengeti Boys wamepoteza mchezo kwa kufungwa magoli 5-4 dhidi ya Nigeria, magoli ya Nigeria yalifungwa na Olatomi dakika ya 20, Wisdom aliyefunga magoli mawili dakika ya 29 na 72, Akinkunmi dakika ya 37 na Jabar dakika ya 78.
Magoli ya Serengeti Boys yalifungwa na Edmund aliyefunga mawili dakika ya 21 na 58 kwa penati, Kelvin John dakika ya 51 na nahodha wao Moris dakika ya 55, Serengeti Boys sasa wana mtihani wa kuhakikisha wanashinda michezo yao miwili ya Angola na Uganda ili kufuzu kucheza nusu fainali na kukata tiketi ya kucheza Kombe la dunia la vijana nchini Peru.
Tatizo kwa Serengeti Boys kupoteza mchezo inaaminika ni kutokuwa na uimara wa safu ya ulinzi lakini sambamba na kuwa na udhaifu wa kukaba pale ambapo wanakuwa hawana mpira, licha ya golikipa wao Mwinyi Yahya kuonekana kama mdhaifu wa kucheza mipira ya mashuti ya mbali, mchezaji wa Nigeria Amoo akiibuka mchezaji bora wa mechi.
Tags