Serikali Kuanza Kuuza korosho Ghafi na Zilizobanguliwa.

Serikali Kuanza Kuuza korosho ghafi na zilizobanguliwa.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imekaribisha wafanyabiashara mbalimbali kununua korosho ghafi na zilizobanguliwa.

Tangazo la TanTrade lililosainiwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha mamlaka hiyo, Theresa Chilambo linaeleza kuwa wanunuzi wanaotakiwa ni wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda, hoteli, maduka ya jumla na rejareja, Supermarket, taasisi za umma na binafsi, vyuo, shule na wananchi.

Uuzwaji wa korosho hizo unakuja ikiwa ni siku chache tangu Rais John Magufuli alipofanya ziara mkoani Mtwara ambako pamoja na mambo mengine, aliitaka Wizara ya Viwanda na Biashara kuuza korosho hizo kwa kuwa kadri zinavyokaa Serikali inatumia gharama kubwa kuzihudumia.

“Wizara ya viwanda imenunua mikorosho imekaa nayo inaiangalia mpaka ikutwe na ya mwaka huu?” Alihoji Rais Magufuli wakati akizindua kiwanda cha kubangua korosho cha Yalini mkoani Mtwara.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad