Serikali kuja na daftari ili kupatikana takwimu za walemavu

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mheshimiwa Stella Ikupa amesema hayo alipokuwa  akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni Mheshimiwa Maulid Mtulia aliyetaka kujua kama serikali inaweza kuorodhesha idadi ya walemavu  nchini kwa kuzingatia makundi yao kwa asilimia.

Mhe. Ikupa amesema kwa mujibu taarifa ya Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 iliyotolea na Ofisi ya Taifa ya Takwimu idadi  ya walemavu kwa makundi  yaani Ualibino, Kuona, Usikuvu, Kutembea, Kukumbuka, Kujihudumia na Ulemavu  mwingine ni milioni mbili laki sita elfu arobaini na moja mia nane na wawili na kwamba katika kuhakisha watu wote wenye ulemavu hasa vijana, watoto,na wanawake hawachiwi nyuma kiuchumi.

Amesema serikali inaendelea kuwajengea uwezo watoto wote wenye ulemavu ikiwa ni pamoja kuwapatia elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa makundi ya vijana na wanawake wenye ulemavu kupitia vyuo vya watu wenye ulemavu na program ya kukuza ujuzi hapa nchini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad