Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, amesema Serikali haijalizuia Shirika la Fedha Duniani (IMF) kuchapisha ripoti ya uchumi wa Tanzania isipokuwa kinachofanyika ni mazungumzo kati ya serikali ya Tanzania na shirika hilo kabla ripoti hiyo haijachapishwa.
Dk. Mpango ametoa taarifa hiyo bungeni leo Jumanne aprili 23, alipokuwa akitoa ufafanuzi wa maelezo ya Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), aliyesema Serikali imelizuia shirika hilo kutoa ripoti ya uchumi wa Tanzania.
Katika maelezo yake Mwakajoka alipokuwa akichangia makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa fedha 2019/20, alisema waandishi wa habari wamejaa hofu ya kuripoti mambo mbalimbali yakiwamo hali ya uchumi wa Tanzania.
Kutokana na hali hiyo alishauri waandishi wa habari waachwe huru ili waripoti mambo mbalimbali kwa maslahi ya umma.
Serikali Yasema Haijaizuia IMF Kuchapisha Hali ya Uchumi wa Tanzania
0
April 23, 2019
Tags