Serikali Yataka Kurahisisha Mazingira Biashara ya Madini

Serikali Yataka Kurahisisha Mazingira Biashara ya Madini
Serikali kupitia Wizara ya Madini inalenga kurahisisha Mazingira ya Biashara ya Madini ikiwemo kuwalea wachimbaji na kuwataka wafanyabiashara na wachimbaji kuhakikisha wanajisimamia wenyewe kwa manufaa yao na Taifa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati alipokutana na Viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa Madini Tanzania (TAMIDA), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Sam Mollel ofisini kwake jijini Dodoma Aprili 10, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu biashara ya madini nchini.

Amekitaka chama hicho kuendelea kushirikiana na wizara kwa lengo la kusukuma mbele Sekta ya Madini ikiwemo kuhakikisha biashara ya madini inafanyika katika mazingira yenye kuzinufaisha pande zote na kuwasisitiza viongozi hao kuhakikisha wanachama wao wanafuata taratibu wanapofanya biashara ya madini.

Awali, kabla ya kujibu hoja zilizowasilishwa na chama hicho, Waziri Biteko amekipongeza  chama hicho kwa kuwa kimekuwa kikitoa njia mbadala pindi kinapowasilisha changamoto na kero  zake badala ya kuishia kulalamika na kuongeza, “wizara inaona fahari kwa hilo na tunayachukulia kwa umuhimu maoni yenu,”.

Akizungumzia suala la kodi ya ongezeko la thamani na kodi ya zuio ambayo imeondolewa kwenye uchimbaji mdogo, Waziri Biteko amekitaka Chama hicho kutoa nafasi kwa serikali kufuatilia suala hilo. Waziri Biteko ameleeza hilo kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa TAMIDA Sam Mollel ambaye ameeleza kuwa, katika mkoa wa Arusha, kodi hiyo bado inatozwa licha ya serikali kuiondoa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad