Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Astashata Nditiye amesema Serikali haijatoa tamko la kupiga marufuku kumiliki laini nyingi za simu badala yake imelenga kuzuia mwananchi mmoja kutumia laini zaidi ya moja, kwa mtandao mmoja.
Naibu Waziri Nditiye ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ambaye alihoji kuhusiana na kauli hiyo iliyotolewa na serikali hivi karibuni.
Mbunge Selasini amehoji kuwa, "Waziri amesema Mei 1, utaanza usajili wa laini za simu kwa alama za vidole, akasema hakuna kumiliki laini 2 mpaka uruhusiwe, haudhani mtawatesa wananchi kwa maeneo ambayo mitandao mingine haipatikani?".
Akijibu swali hilo ndani ya Bunge Naibu Waziri amesema kuwa, "nilichosema ninatamani kila mtanzania awe na laini moja kwaa kila mtandao, akitaka laini nyingine aseme tu, tunaepuka utitiri wa laini nyingi, mfano ' Zile laini za tuma kwa namba hii ni laini zisizo na tija'".
Serikali Yatolea Ufafanuzi Umiliki wa Laini za Simu Zaidi ya Moja
0
April 23, 2019
Tags