Simba Mkubwa Kabisa Agunduliwa Kenya

Simba mkubwa kabisa agunduliwa Kenya
Utafiti mpya umebaini kwamba mmoja wa wanyama wakubwa kabisa anayekula nyama aliishi nchini Kenya yapata miaka milioni 23 iliyopita.

Mnyama huyo aliyepewa jina la "Simba Mkubwa Kutoka Afrika", alitambuliwa kutokana na meno na mabaki ya mifupa iliyozikuliwa magharibi mwa Kenya miongo kadhaa iliyopita.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Ohio nchini Marekani wanaamini mnyama huyo alikuwa mkubwa zaidi kuliko simba wa sasa na hata kuliko dubu.

Ushahidi wa mabaki hayo unaonesha kuwa huenda simba huyo aliishi kwa kuwinda na kuwala wanyama wa jamii ya tembo na viboko ambao walikuwapo kwenye eneo hilo katika zama hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad