'Sio Sahihi kwa Mawaziri Kujibu Ripoti ya CAG'


Mwenyekiti wa PAC Naghenjwa Livingstone Kaboyoka  ameeleza kuwa si sahihi kwa mawaziri kujibu hoja za CAG na kwakufanya hivyo ni kinyume Cha taratibu. Hii inakuja siku moja baada ya Waziri Lugola kueleza mbele ya Spika kwamba CAG ni mwongo.

Ameeleza kuwa kwenye Public Audit Act kifungu cha 38 (1) na (2) pia kwenye Kanuni ya Katiba inawapa mamlaka PAC na LAAC kuzungumzia juu ya taarifa za CAG na kuna utaratibu wake wa namna ya kujadili taarifa hizo.

"Sio sahihi kwa mawaziri kujibu ripoti ya CAG, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha taratibu, na kama taratibu zisipofuatwa, nchi hii haitatawalika. Kaboyoka amesema kuwa CAG ni jicho la Bunge na wala sio adui wa serikali." ameeleza.


"Mpaka taarifa ya CAG inafika Bungeni inamaana Serikali au Maafisa Mazuhuri wameshindwa kujieleza na CAG ameona hilo ni tatizo. CAG anapopata taarifa anawapa siku 21 Maafisa Mazuhuri kujieleza, yale wanayoshindwa kutolea ufafanuzi ndio CAG anayaleta Bungeni," amesema.

Aidha, amesema kuwa Mtu yeyote anayejibu hoja za CAG kinyume na taratibu zilizowekwa na Bunge, basi atakuwa hajibu hoja za CAG za ripoti yake iliyofungwa Juni 30, 2017 bali atakuwa anajibu kitu kingine.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad