Uongozi wa soko la Mbezi jijini Dar es salaam umeeleza kusikitishwa kwake na kukosekana kwa huduma ya choo ndani ya soko hilo kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Akiongea na Kurasa leo, Katibu wa soko hilo amesema ukosefu huo wa choo umesababisha kuwepo kwa uchafuzi wa mazingira unaotokana na watu kujisaidia hovyo.
Kwa upande wao wafanyabiashara wenyewe wameeleza hofu waliyonayo ya kuugua magonjwa ya milipuko huku wengine wakieleza kwamba wanalazimika kujisaidia kwenye mifuko ya plastiki.