Spika Ametangaza Deni Analodaiwa Mbunge Lema

Spika Ametangaza Deni Analodaiwa Mbunge  Lema
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ametangaza deni analodaiwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambalo ni zaidi ya shilingi milioni 200 kuwa huenda ni sababu inayomfanya Mbunge huyo kutokuwa sawa hivi sasa.


Spika Ndugai ametangaza deni hilo katika muendelezo wa vikao vya Bunge Jijini Dodoma, wakati akielezea uamuzi wa kumtaka Mbunge Lema kufika kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, kujibu madai ya kuunga mkono kauli ya kuwa Bunge ni 'dhaifu'.

Spika Ndugai amesema, "yapo mambo ambayo hawayasemi ngoja tuseme kidogo, amekopa milioni 644, sasa hivi ameshalipa zimefika milioni 419, huu ni msongo wa mawazo ndiyo maana anajilipua na kadhalika".

Akitangaza uamuzi wa kumtaka Lema kwenda Kamati ya Maadili Ndugai amemtaka afike kwenye kikao saa 8 mchana na kesho itakuwa hatma yake.

Mapema jana Kamati ya Maadili, ilitangaza kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali, CAG Prof Assad na kutangaza kumsimamisha mikutano miwili Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad