Spika Ndugai Atumiwa Barua Kisa CAG

Taasisi ya Change Tanzania imetuma maombi kwa Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai kuangalia upya maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge juu ya uamuzi wa kutofanya kazi na Mdhibiti na Mkaguzio wa Hesabu za Serikali Prof Assad uliofikiwa April 2 2019.


Kupitia barua yao maalum waliyoituma kwa Spika wa Bunge wa Tanzania Taasisi hiyo imesema imekusanya maoni ya wananchi waliofikia 15000 ambao wameonesha kutoridhidhishwa na maamuzi hayo ya Bunge.

"Tunaambatanisha sahihi pamoja na maoni ya wananchi takribani 15,000 waliotia sahihi wito kutoa azimio la kutofanya kazi na CAG, wito unaendelea kuungwa mkono siku hadi siku na tunaamini kuwa itazidi kuongezeka, kama tulivyoainisha katika wito wetu, sisi wananchi tunakuomba Mheshimiwa Spika na Kamati ya Maadili kurejea maamuzi yenu kuhusu azimio la kutofanya kazi na CAG".

"Hadhi na heshima ya Bunge inatokana na kazi yenu nzuri ya kuisimamia Serikali kwa niaba yetu, watanzania tungependa kuendelea kuona Bunge likidumisha mfumo huu wa uwajibikaji na utawala bora kama kawaida yake."

"Hivi sasa tunatumia mfumo maalum wa wito (petition) ikiwa ni njia nzuri ya kisheria na kistaarabu kuelekeza maoni, maombi na changamoto zao kwa viongozi" imemaliza taarifa hiyo na kusainiwa na Mbaraka Islam ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo. imemaliza taarifa hiyo


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad