Sri Lanka Laomboleza Kifaifa Mazishi ya Ndugu Zao 300

Sri Lanka imefanya mazishi ya pamoja ya waathirika wa mashambulio ya mabomu yaliyotokea Jumapili na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 300 ikiwa ni pamoja na kuadhimisha siku ya kitaifa ya maombolezo kwaajili ya kuwakumbuka wote waliopatwa na mkasa huo.


Mashambulio hayo mfululizo yalitokea katika makanisa na hoteli huku yakiwaacha watu wengine 500 majeruhi kwa niaba ya Polisi.


Kabla ya tukio hilo Taifa hilo pia lilipitia kipindi cha ukimya wa dakika tatu na kutangazwa kwa hali ya hatari ili kujilinda zaidi na mwendelezo wa mashambulizi yanayoweza kujitokeza.


Serikali ya Sri Lanka imekilaumu kikundi cha Kiislamu cha nchini humo cha National Thowheed Jamath (NTJ) kwa kuhusika na mashambulio hayo.Mpaka sasa polisi nchini humo wanawashikilia washukiwa 40 wanaohusishwa na matukio hayo ya mashambulizi.

Msemaji wa Serikali hiyo amesema miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na Raia wa Syria.


Katika hatua nyingine waziri wa ulinzi wa nchi hiyo, Ruwan Wijewardene ameliambia Bunge leo, Jumanne kuwa “uchunguzi wa awali” unaonesha kuwa milipuko hiyo mfululizo inauhusiano na kisasi cha kushambuliwa kwa msikiti huko Christchurch, New Zealand, mwezi Machi. Hakutoa taarifa zaidi juu ya hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad