Suala la kusajili laini upya, TCRA waeleza sababu

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema lengo la mfumo mpya wa usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole linatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wananchi waliosajili laini kwa kutumia vitambulisho feki. 


“Kuanzia Mei Mosi mwaka huu, wananchi wote wanatakiwa kusajili laini zao kwa mfumo huo, na laini ambazo hazitasajiliwa zitafungiwa pindi tutakapotangaza muda wa ukomo. 


“Tunatambua kwa kutumia mfumo huu, itaondoa udanganyifu mkubwa unaosababisha kuwepo kwa ugumu wa TCRA katika kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa kutumia mitandao,” amesema Mhandisi Mihayo. 


Aidha Mihayo amesema katika mfumo huo wananchi watatakiwa kwenda na kitambulisho cha uraia au namba ya kitambulisho kwa ajili ya kusajili laini zao. 


Hayo yamelezwa leo na Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo, wakati wa kuzindua kampeni ya kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa mfumo huo mkoani wa Simiyu. 


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad