Tanzania Yapanda Nafasi 6 Viwango vya FIFA

Tanzania Yapanda Nafasi 6 Viwango vya FIFA
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kupanda nafasi sita katika listi ya viwango vya Shirikisho la Soka Duniani FIFA vya mwezi April.

Katika viwango hivyo, Taifa Stars imepanda kutoka nafasi ya 137 mwezi uliopita hadi nafasi ya 131 mwezi huu.

Kuongezeka kwa nafasi hizo kumetokana na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania kufuzu fainali ya AFCON dhidi ya Uganda, Machi 24, ambapo Taifa Stars ilishinda kwa mabao 3-0.

Ukiachana na Taifa Stars, nchi nyingine ya Afrika Mashariki ambayo imeongeza nafasi katika listi hiyo ni Burundi ambayo imepanda nafasi mbili hadi nafasi ya 136 kutoka nafasi ya 134 mwezi uliopita, huku timu timu ya taifa ya Uganda ikishuka kwa nafasi mbili hadi nafasi ya 78.

Timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' imeshuka nafasi mbili nyuma hadi nafasi ya 108, Rwanda ikishuka nafasi tatu hadi nafasi ya 138 huku Sudani Kusini ikishuka kwa nafasi tatu hadi nafasi ya 167.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad