Hatua ya upangaji wa makundi ya michuano ya Afcon ya Afrika imepangwa jana nchini Misri ambapo tayari Tanzania imewajua wapinzani wake watakaomenyana nao mwezi Juni nchini Misri.
Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia pamoja na Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania, Emmanuel Ammunike ilishuhudiwa na Dunia nzima kupitia SuperSport
Tanzania ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza fainali hizo baada ya miaka 39, imepangwa Kundi C na timu za Senegal, Algeria na Kenya.