Tcra Yatoa Elimu Juu ya Usajili wa Laini za Simu

Tcra yatoa elimu juu ya usajili wa laini za simu
Kanda ya Mashariki ya Mamlaka ya Mawasiliano Nchini(TCRA) imeendelea kutoa elimu ya mawasiliano nchini ikiwa ni pamoja kuwataka wananchi wasajili namba zao kwa kutumia alama za
vidole.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyandira mkoani Morogoro Mkuu wa Kanda ya Mashariki ya Mamlaka hiyo Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa serikali imeshatangaza wananchi juu ya usajili wa namba za simu kwa alama za vidole hivyo ni vyema wasajili kwani baada ya muda uliowekwa ukimalizika namba za simu zisizosajiliwa zitafungwa na watoa huduma.

Odiero amesema kuwa usajili huo ni usalama kwa mtumiaji wa mawasiliano ambapo kwa alama hizo hawawezi kuingiliana na mtu mwingine yeyote duniani.
Amesema kuwa wananchi watumie mawasiliano kwa mujibu wa sheria zilizopo bila na mtu atakaye kwenda kinyume na sheria zilizowekwa anaweza kufungwa jela au faini na wakati mwingine ni faini pamoja na kifungo kwa wakati mmoja.

Odiero amewasaa wananchi wa Nyandira kutumia simu kwa kutengeneza ajira kwani mawasiliano yanarahisha kufanya biashara na kuweza kujiingizia kipato.
Aidha amesema kuwa kitambulisho kinachotakiwa ni cha uraia /kitambulisho cha Taifa na serikali imetoa vitambulisho hivyo na inaendelea kutoa kwa wale wasiokuwa navyo wafuatilie mamlaka husika na kuweza kuwa navyo na hatimaye kujisajili namba za simu kwa alama za vidole.

Hata hivyo amesema kuwa mtu anaweza kuwa na laini moja au zaidi isipokuwa hawezi mtu kumiliki laini mbili kwa mtandao mmoja.
"Tumejipanga kuhakikisha wananchi wetu tunawafikia popote mlipo ili kuwapa elimu ya mawasiliano msiweze kupata changamoto katika kutumia mawasiliano hayo"amesema Odiero.
Katika utoaji wa elimu kwa wananchi kanda hiyo pia inatoa elimu kupitia vituo radio pamoja na Luninga ili kwa wale wasiweza kufika katika mihadhara hiyo kupata taarifa katika vyombo vya habari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad