NA FAUSTINE GIMU GALAFONI,DODOMA
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kanda ya kati imeziagiza kampuni za mawasiliano kuzuiya meseji za matapeli zinazotumwa kwa watu kabla hazijafika kwa wananchi ili kudhibiti matukio ya namna hiyo.
Pia mamlaka hiyo imesema ili kukabiliana na makoa ya mtandao watapambana na kampuni za mawasiliano nchini pindi watakapobaini mtu anatumia line bila kusajiliwa kwa mfumo wa alama za vidole.
Mkuu wa TCRA kanda ya kati Dodoma Antonio Manyanda ameyasema hayo jijini hapa wakati wa mkutano wa wadau wa huduma za mawasiliano mkoani hapa ulioandaliwa na maamlaka hiyo kwa lengo la kujadili changamoto zilizopo pamoja na kuangalia namna ya kukabaliana nazo.
Akifungua mkutano huo kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema wahalifu hao wana mtandao mkubwa hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini ili kuepuka kutapeliwa huku akisema wapo ambao wanatuma meseji wakitumia majina ya viongozi wakubwa ili kutapeli.
Muroto ametumia nafasi hiyo kuwatahadharisha wale wote wanaojihusisha na utapeli kupitia mitandao ya mawasiliano kuwa pindi watakapokamatwa watashughulikiwa bila kigugumizi.
Amesema wanaangalia namna ya kupunguza kama si kumaliza kabisa makosa ya mtandao kwani kwa sasa uhalifu umehamia kwenye mitandao ya mawasiliano na kuwa wamejipanga ukabiliana na watu wa aina hiyo.