Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amedai kuwa tangu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi wazazi wake na familia wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa sana.
Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Septemba 7, 2017 alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi akitokea Bungeni Jijini Dodoma.
"Shida inayo nikabili kwa sasa ni kwamba, toka Mh Lissu ameshambuliwa kwa risasi,wazazi wangu/familia yangu wamekuwa wakiishi kwa shida sana kwa kufuatilia mienendo yangu kila mara. Maisha yetu yamekuwa magumu sana, lakini tumaini langu ni kwamba uovu haujawahi kufanikiwa," ameandika Lema kwenye mtandao wa Twitter.
Utakumbuka April 4 mwaka huu Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ilimtia hatiani Godbless Lema kwa kudharau Bunge kwa kuita Bunge ni dhaifu na hivyo kupewa adhabu ya kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge kuanzia siku hiyo.
Toka Lissu ameshambuliwa familia yangu imeishi kwa shida - Godbless Lema
0
April 18, 2019
Tags