Mamlaka ya bandari nchini TPA imezita taasisi zote zinazofanya kazi bandarini kuhakisha wanafanya kazi kwa saa 24 katika msimu huu wa pasaka na watafanya operesheni maalum kubaini taasisi ambazo hazitatoa huduma na hawatasita kuchukua hatua stahiki dhidi yao.
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa TPA Mhandisi Deusdediti Kakoko jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya bandari na mikakati iliyopo sasa.
Aidha mkuu huyo amebainisha njama chafu ambazo zimepangwa na baadhi ya watu kutaka kutorosha makontena ya mizigo katika sikukuu hizi za pasaka ambayo imeagizwa na nchi za jirani.
Kuhusu hali ya mizigo bandarini amesema kwa sasa mizigo ni mingi kiasi kwamba wamelazimika kubuni sehemu zingine za kuhifadhia mizigo hiyo.