Trump Atakiwa Awasilishe Kodi ya Mapato ya Miaka 6

Trump atakiwa awasilishe kodi ya mapato ya miaka 6
Mwenyekiti wa kamati ya bunge nchini Marekani ameiomba rasmi Idara ya Mapato ya Ndani (IRS) kuwasilisha nyaraka za miaka sita za kodi ya mapato ya Rais wa Marekani Donald Trump pamoja na kodi ya mapato ya baadhi ya biashara zake binafsi, huku wanasiasi wa chama cha Democratic wakijaribu kuchunguza shughuli zake za kifedha.

 Ombi hilo la mwakilishi wa Massachusetts, Richard Neal anaeongoza kamati ya kodi ya mapato, ni la kwanza katika kipindi cha miaka 45 kwa rais ambaye bado yupo madarakani.

 Hatua hiyo isiyokuwa ya kawaida inaweza kuzua mgogoro wa kisheria kati ya serikali ya Trump pamoja na chama cha Democratic kinachodhibiti bunge.

 Neal amezitaka nyaraka hiyo za kodi ya mapato ya miaka sita ya Trump ziwasilishwe kabla ya Aprili 10.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad