Mbunge wa Chama wa Wananchi (CUF), jimbo la Wungwi visiwani Pemba, Juma Kombo amehoji juu ya majibu ya Serikali kuwa mpaka sasa imemkamata mtu mmoja tu anayetuhumiwa kwa matukio ya upoteaji wa watu ambayo yalikuwa yakitokea hivi karibuni.
Akihoji kipindi cha maswali na majibu kwenda kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbunge huyo wa CUF amedai katika jimbo lake kuna vijana ambao hawajulikani walipo mpaka sasa.
Mbunge huyo CUF amesema kuwa "kuna matukio mengi likiwamo la Tundu Lissu na Mohammed Dewji, lakini mtaa wa Mtambwe Pemba, kuna vijana saba walitekwa na matukio mengi halafu mnasema anashikiliwa mtu mmoja,"
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema Serikali Hamad amesema kwa kutumia taarifa za kiintelejensia hadi sasa imefanikiwa kumkamata mtu mmoja kwa makosa ya utekaji nyara.
"Matukio haya kila moja jeshi la polisi linachukua hatua mbalimbali za upelelezi na mengine utetezi umekamilika, kuyazungumzia kwa pamoja inakuwa ni changamoto, ila kwa kuwa suala la upelelezi ni mchakato, itafikia hatua nzuri na haki itapatikana." amesema Masauni.