'Tutawachunguza tu' - TAKUKURU

'Tutawachunguza tu' - TAKUKURU
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini imesema haitaacha kumchunguza mtu yeyote ambaye ataonekana anamiliki mali kuliko kipato chake cha kawaida.

Mkurugenzi wa Uplelezi kutoka TAKUKURU, Kassim Ephrem, ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio ambapo amesema ni ajabu utakuta mtu mwingine anapewa zawadi lakini anashindwa kueleza kwanini amepewa.

"Mtumishi wa umma akipewa zawadi ambayo itaonekana inazidi kipato chake, sheria inamtaka atoe taarifa kwa mabosi wake, umepewa V8 halafu unasema ni zawadi tu na kiongozi wako hukumpa taarifa tutakuchunguza tu." amesema bosi huyo wa TAKUKURU.

"Kuna kesi nyingine tumepeleka Mahakama za Mafisadi kwa kuzishtaki kampuni, na wengi wanashtakiwa kukwepa kodi au kushindwa kutumia mashine za EFD" ameongeza bosi huyo wa TAKUKURU

Aidha bosi huyo wa TAKUKURU ameongeza kuwa, "walipa kodi ni wananchi ambao ni wateja wetu wakiripoti eneo fulani kuna rushwa, huwa hatumtaji kwa sababu sheria haituruhusu, ila kuna muda tunapita kutoa elimu kwa umma kuwa ukinunua kitu dai risiti
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad