Chama cha soka Ulaya UEFA kimetangaza kuipiga faini club ya Chelsea kufuatia tukio lililotokea wakati wa mchezo wa UEFA Europa mwezi February ugenini dhidi ya Malmo, UEFA wamefikia hatua ya kuipiga Chelsea faini ya pound 11,100 ambacho ni zaidi ya Tsh milioni 33 kwa kosa la shabiki wao.
UEFA imewapiga Chelsea faini hiyo kwa kosa la mashabiki wao kuingia uwanjani wakati wa mchezo, tukio hilo lilitokea katika mchezo wa 32 bora ya UEFA Europa League dhidi ya Malmo ambapo Chelsea walishinda kwa magoli 2-1.
Club zote Chelsea na Malmo vimepigwa faini kwa mashabiki wao kutupa vitu uwanjani wakati wa mechi, Malmo nao wamekutwa na adhabu ya kupigwa faini ya pound 49000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 148 kwa makosa ya mashabiki wao kurusha miale ya moto uwanjani wakati mchezo ukiendelea.