Muongozaji mkongwe wa filamu nchini Marekani John Singleton amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.
A
John (51) alikuwa kwenye ‘Life support’ kwa siku kadhaa katika chumba cha uangalizi wa wagonjwa mahututi hospitali mjini Los Angeles. Familia yake imethibitisha kifo chake baada ya kuondolewa kwenye mashine hiyo usiku wa kuamkia leo.
Umaarufu wake umebebwa na filamu kubwa ambayo aliiongoza mwaka 1991 ‘Boyz N the Hood’ iliowakutanisha wakali kama Ice Cube, Nia Long na wengine. Filamu hii ilimuingiza kwenye historia ya kuwa mtu mweusi wa kwanza mwenye umri mdogo (24) kuwa nominated kwenye tuzo kubwa za filamu, Academy Awards.
Kauli ya familia yake ilikuwa hivi: “an agonizing decision, one that our family made over a number of days with the careful counsel of John’s doctors.”
Ugonjwa wa Kiharusi wasababisha kifo kwa muongozaji mkongwe wa Movie Marekani
0
April 30, 2019
Tags