Uingereza Kujitoa Umoja wa Ulaya Usiku wa Kesho, Mkutano wa Dharura Wafanyika Kuongeza Muda wa Brexit

Uingereza kujitoa umoja wa Ulaya usiku wa kesho, mkutano wa dharura wafanyika kuongeza muda wa Brexit
Umoja wa Ulaya umefanya mkutano wa dharura hapo jana kuamua ni kwa muda gani ucheleweshwaji wa Brexit utatolewa kwa waziri mkuu wa Uingereza Theresa May na kwa masharti gani.


Bila ya kuahirisha Uingereza itajitoa kutoka Umoja wa Ulaya bila makubaliano usiku wa manane siku ya Ijumaa hali ambayo inaweza kuzusha mkanganyiko wa kiuchumi.

May anataka kuahirisha Brexit kutoka Aprili 12 hadi Juni 30 ili kuweza kutayarisha kujitoa kwa utaratibu mzuri , lakini viongozi wa Umoja wa Ulaya waliokusanyika mjini Brussels kwa ajili ya mkutano huo wanatarajiwa kumpa muda mrefu zaidi wa uchelewesho, wa hadi mwaka mmoja.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliliambia bunge mjini Berlin kabla ya kwenda Brussels kwamba viongozi huenda wakaunga mkono ucheleweshwaji huo kwa muda mrefu kuliko waziri mkuu wa Uingereza alivyoomba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad