Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ametoa onyo kali kwa watu wenye tabia za ubakaji na udhalilishaji wa kingono kwa watoto na wanawake, na kusema kwamba kwamba kwenye wilaya yake iwapo mtu atakamatwa hatopewa dhamana.
Akizungumzia hilo mbele ya umati uliokuwa ukimsikiliza mapema leo, Jerry Muro amesema kwamba mtu yeyote atakayekamatwa kwa makosa ya ubakaji na udhalilishaji wa kingono, ajue wazi kuwa hatopata dhamana akiwa kituoni, labda iwe mbele ya mahakama.
“Watu wenye vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watoto, wanawake na kina mama, katika Wilaya yetu huna dhamana, utakapopelekwa kituo cha polisi, tunajua dhamana ni haki yako, lakini katika hili Arumeru tumejiwekea utaratibu, hautapata dhamana, utashikiliwa mpaka kesi itakapokwisha, polisi huku tutakushikilia, hautapewa dhamana kituo cha polisi, omba Mungu ukapewe dhamana mahakamani kama utapelekwa mahakamani ukapewa dhamana mahakamani”, amesema Jerry Muro
Akiendelea kuzungumzia hayo Jerry Muro amesema kwamba iwapo atalalamikiwa kukiuka kwa haki za binadamu kwa kumnyima dhamana mbakaji, ni vyema wakajiuliza iwapo haki hizo zinaruhusu kufanya maovu hayo, na iwapo hairuhusu basi wajue wazi kuwa hata wao hakli yao ya dhamana haitapatikana.
“Hatufanyi hii kukiuka haki za binadamu, hakuna haki za binadamu inayoruhusu mtu mzima kumuingilia mtoto mdogo, kwa hiyo usitafute haki za binadamu wakati nimesha kukamata, kabla hujatafuta haki za binadamu, jiulize kwanza kabla ya kwenda kubaka mtoto, je haki za binadamu zinaruhusu kwenda kubaka mtoto, kama haziruhusu kubaka mtoto haki hizo hizo za binaadam hazitaruhusu mimi kukupa dhamana”, amesema Jerry Muro.
Jerry Muro pia amezidi kuwasisitiza vijana waendesha boda boda wa ndani ya mkoa huo kujiepusha na vitendo hivyo, kwani wamekuwa wakisifika kwa kufanya maovu kumalizia 'handasi' zao kama alivyoitaja.