Umoja wa Afrika watoa wito kwa Sudan

Rais wa baraza la Umoja wa Afrika, Musa Faki Muhammed, amezitaka pande zote nchini Sudan kufikia makubaliano ya kuweka serikali ya muda ya kiraia, ambayo itaongoza nchi hio kufanya uchaguzi katika hali ya uadilifu, haki na uwazi.

Muhammed ambaye alifanya ziara ya siku mbili nchini Sudan, baada ya ziara hiyo aliaandaa taarifa yake ya maandishi. Katika taarifa hiyo alisema kwamba alipata kukutana na  wajumbe wa baraza la kijeshi linaloongoza serikali ya mpito, pia alikutana na vyama vya kisiasa na makundi ya kijamii kufanya nao mkutano wa kiushauri.

Muhammed,  alisema kwamba wadau wote nchini Sudan kwanza kabisa wanapaswa kuweka mbele maslahi mapana ya Sudan.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad