Mkuu wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker amesema kwamba makampuni ya Ulaya yanapaswa kupata haki sawa nchini China kama makampuni ya China yanavyopata katika bara la Ulaya.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Deutsche Welle, Juncker ameyasema hayo hapo jana wakati wa mkutano ambao umekuwa na hali ya wasi wasi kuliko ilivyo kawaida kati ya Umoja wa Ulaya na China ukianza mjini Brussels.
Mkutano wa Umoja wa Ulaya na China wa kila mwaka unawakutanisha pamoja kiongozi mkuu wa pili wa China na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya unatumika kama kielelezo cha hali ya mahusiano kati ya Ulaya na taifa hilo kubwa la bara la Asia.
Mkutano wa mwaka huu unakuja mwezi mmoja baada ya halmashauri ya Umoja wa Ulaya, kitengo cha utendaji cha Umoja wa Ulaya, kuieleza China kama mshindani wa kimfumo katika ripoti maalum yenye vifungu 10 ambayo ilisisiza kukosekana kwa hiari upande wa China, kuchukua hatua zenye uwiano wa haki katika biashara.
Umoja wa Ulaya wataka haki sawa zakibiashara na China
0
April 10, 2019
Tags