Uongozi wa Yanga Waja na Suluhu ya Kufungwa na Mtibwa

Uongozi wa Yanga Waja na Suluhu ya Kufungwa na Mtibwa
Uongozi wa klabu ya Yanga umefunguka juu ya mustakabali wa sasa wa klabu hiyo kufuatia kupoteza dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu katikati ya wiki.

Yanga kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Omary Kaaya, imesema kuwa inafahamu kuwa kupoteza kwa mchezo huo hakujawafurahisha mashabiki wa klabu hiyo na kuwataka kutokata tamaa katika mbio za kuwania ubingwa.

"Tunajua kuwa hizi mbio za ubingwa ni vita na unapoteleza ni vyema kusimama na kuangalia wapi umejikwaa ili uweze kupambana kuelekea kwenye ubingwa", amesema Kaaya.

Kaaya ameongeza kuwa, "ni kweli haitupi mazingira mazuri sana lakini safari bado ni ndefu na tutaendelea kupigana, naamini benchi la ufundi likiongozwa na mwalimu wetu wameona mapungufu na watayafanyia kazi".

Yanga ilipoteza mchezo wake na Mtibwa Sugar na kuifanya kusalia na pointi zake 74 baada ya kucheza mechi 23. Azam FC inakamata nafasi ya pili ikiwa na alama 66 katika michezo 31 huku Simba ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 60 baada ya kucheza mechi 23.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad