Uwanja mpya wa Tottenham washika nafsi ya pili kwa ukubwa London, Hazard aumwagia sifa

Klabu ya Tottenham Hotspurs’ tayari imeufungua uwanja wake mpya ambao ulianza kujengwa mwaka 2016 ukiwa na uwezo wa kuingiza watu elfu 62062, Ukiwa ni uwanja wa pili katika jiji la London kuingiza watu wengi baada ya Wembley kuingiza watu elfu 90000. Uwanja wa Tottenham una urefu wa mita 105 na upana wa mita 68 sawa na yad (114.8 kwa 74.4).
Uwanja huu ukiwa umegharimu $ bilion 1.3 wakiupa jina la TOTTENHAM HOTSPUR STADIUM ambalo ni jina la muda kwani wanatarajia kulibadili jina hili Ingawa mashabiki wa timu hiyo wanapendekeza Uitwe “NEW WHITE HART LANE STADIUM”



Tottenham Hotspur ilijipatia rekodi iliovunja rekodi ya dunia ya £113m baada ya kodi msimu uliopita. Fedha hizo zimeshinda faida ya £106m ilizopata Liverpool mapema mwaka huu.

Matokeo ya kila mwaka ya kifedha ya msimu 2017-18 yanaonyesha kwamba mapato ya Spurs yalipanda kutoka £310m hadi £380m kutokana na mauzo ya wachezaji, mashabiki wengi waliojitokeza katika uwanja wa Wembley na kufuzu katika awamu ya muondoano ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad